Jukwaa huru la kidijitali linalowaunganisha Wachaga wote ndani na nje ya Tanzania kwa lengo la kuhifadhi utamaduni, kuimarisha mshikamano, na kuchochea maendeleo ya pamoja.
Chagua kiwango kinachokufaa na uanze kukua pamoja nasi
Chagua eneo unalolipenda kushiriki - kila moja lina maelezo ya kina na utaratibu wake maalum
Ni Mpango wa kuinuana kifedha kwa Mzunguko wa Michango ya kila Siku.
Umoja wa Shida na Raha - kusaidiana katika shida na kushirikiana katika furaha.
Jiunge na majadiliano na upate taarifa kwa wakati halisi.
Mbinu mbalimbali za upatu zinazotumika kwa sasa.
Semina na mafunzo mbalimbali kwa ajili ya jamii.
Fursa za kiuchumi na kimaendeleo kwa Wachaga.
Tunajenga jamii yenye mshikamano imara na maendeleo endelevu
Kuwa jukwaa linaloongoza kwa kuwaunganisha Wachaga duniani, kuhifadhi utamaduni wetu tajiri, na kujenga jamii yenye mshikamano imara na maendeleo endelevu.
Kuunda mfumo shirikishi unaowawezesha Wachaga kubadilishana uzoefu, maarifa na rasilimali kwa lengo la kuinua hali ya maisha ya kila mmoja na jamii kwa ujumla.
Uwazi, Uwajibikaji, Mshikamano, Usalama, Nidhamu na Ushirikiano - ndio nguzo zinazotuongoza katika kila tunachofanya.
Mkombozi wa kiuchumi kwa akina mama na vijana wenye maono ya mafanikio.
Inawapa akina mama uwezo wa kupata mitaji ya mzunguko kila siku bila riba wala masharti magumu, kukuza biashara zao na kuleta heshima ndani ya familia kupitia mshikamano.
Sisi kwa Sisi inageuza mzunguko wa siku 100 kuwa daraja la vijana kuanzisha miradi mipya. Ni shule ya nidhamu ya kifedha inayokuandaa kuwa mfanyabiashara mkubwa wa kesho.
Wanachama wanapata uwezo wa kufanya uwekezaji ambao peke yao isingekuwa rahisi. Huu ni mkakati wa dhati wa kukuza mzunguko wa pesa (Cashflow) kwa kila mwanajamii.
Kuwa sehemu ya jamii inayothamini utambulisho, mshikamano na maendeleo ya pamoja. Wachagawote ni jukwaa huru la kidijitali linalowaunganisha Wachaga wote duniani kote.
Iwe unatafuta kujiunga na Sisi kwa Sisi au USHIRA – tunakukaribisha kwa mikono miwili.
Kumbuka: Sisi kwa Sisi si mkopo wala uwekezaji. Ni makubaliano ya hiari ya kukua pamoja.